Nchini kenya, bibi mmoja mwenye umri
wa miaka 100 amefungwa jela kwa kosa la kukiuka amri ya mahakama kwenye
sakata inayohusu ugavi wa ardhi ya jamii.
Ni nadra sana nchini
Kenya kwa mtu wenye umri mkubwa kama huo kufungwa jela na huenda hatua
hii ikapokelewa kwa mshangao mkubwa na wananchi.Ngima Gakoromo mwenye umri wa miaka 100 na watoto wake wawili wa kiume kwa sasa wamekamilisha siku 6 katika jela ya Embu kati mwa Kenya.
Hakimu mkaazi wa Embu, Florence Muchemi alimpata bibi huyo na hatia ya kutotii amri ya mahakama ya kumpa kipande cha ardhi
Justa Wawira, ambaye alikuwa ameishawishi mahakama kwamba anastahili kupata sehemu ya samba la jamii.
Bibi huyo alipelekwa korokoroni baada ya kukosa kulipa faini ya shilingi laki moja za Kenya sawa na dola alfu 1100 za marekani.
Lakini watoto wake hawakubahatika- walihukumiwa miezi sita jela kila mmoja bila faini.
Wachunguzi wa mambo wanasema huenda kufungwa huko kwa nyanya huyo kukazua hisia kali ikizingatiwa umri wake mkubwa wa karne moja
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni