Mtandao wa kuwakutanisha wapendanao na unaowalenga watu walio katika ndoa nchini Ufaransa umeshtumiwa kwa kuvunja sheria.
Mahakama moja nchini Ufaransa sasa inatarajiwa kuamua iwapo mtandao huo unawafanya wanandoa kufanya udanganyifu.Je, inakubalika kuwepo kwa mtandao unaokuza uashereti,ambapo uaminifu katika ndoa umewekwa katika sheria za taifa hilo?
Hilo ni swali linalokabili kampuni ya Gleeden ambayo inasifika kwamba ndio kampuni inayowapatia wanawake raha za ziada za nje ya ndoa.
Muungano wa familia za kikatoli ambao umekasirishwa na matangazo ya kampuni hayo umefungua kesi dhidi yake likitaka kujua uhalali wa mtandao huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni