17 Machi 2015
Mtoto mwenye miaka 3 ana uwezo wa kufanya hesabu za Sekondari na kuongea Kiingereza vizuri
Nilikuwa naperuzi kwenye mitandao maarufu nchini nikakutana na hii habari inayomuelezea huyu Mtoto pichani ambaye ana miaka 3 anaitwa Nice, ana uwezo wa kufanya hesabu za Sekondari kwa uwezo wa kutisha na kuongea kiingereza fasaha kabisa bila kigugumizi. Lakini kichekesho ni kwamba tangu azaliwe hajawahi kwenda shule au kuhudhuria darasa la aina yoyote.
Hawa ni wale watoto wenye vipaji maalumu hivyo serikali inaweza hata isimsaidie ili kuweza kumwendeleza na hatimae kutimiza ndoto zake na sio kuishia kumwona kwenye vyombo vya habari kisha mwisho wa siku tusijue alipo ishia ni wakati wetu sasa wa kumsaidia maana watoto kama hawa wapo wengi sana mitaani hasa maeneo ya vijijini ila huwa hamna wa kuwaendeleeza na mwisho wa siku hupoteza uwezo wao mkubwa walio zaliwa nao ushauri wangu ni ndio huu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni