Siasa za Tanzania kwa hivi sasa zimechukua mkondo mpya baada ya
aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kujiunga rasmi na
chama alichokuwa akihusishwa kwa muda mrefu, chama cha ACT-Tanzania.
Mwanasiasa huyo ambaye jana alikutana na waandishi wa habari na kueleza
sababu za kujiunga na chama hicho amekuwa akijadiliwa katika kona
mbalimbali kutokana na hatua yake hiyo ambayo wengine wanaitizama kama
ni hatua itakayokoleza ushindani mkali kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao.
Miongoni mwa watu wanaotajwa kuasisi chama hicho kipya ni msomi wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Kitila Mkumbo ambaye pia amewahi kuwa
kiongozi ndani ya CHADEMA kabla ya kutimuliwa kwa madai ya kuandaa
mkakati wa kuleta mapinduzi katika chama hicho. Una maoni gani kuhusu
uwepo wa chama hicho kipya katika uwanja wa siasa za vyama vingi nchini
Tanzania.
23 Machi 2015
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni