
Polisi nchini Marekani imesema muuaji wa Waandishi wawili wa habari nchini Marekani amefariki.
Ujumbe
unaoonekana kutumwa na mtu aliyekuwa na silaha nchini Marekani na
kuwaua kwa risasi watangazaji hao wawili wa televisheni wakati wa
matangazo ya moja kwa moja unaashiria kwamba alikuwa na uchungu kwa
kinachoonekana kuwa ubaguzi wa rangi.