27 Agosti 2015
Uchaguzi 2015: Jackline Wolper Atangaza Kujiita ‘Jackline Lowassa
Mastaa wa Bongo Movies, Jackline Wolper , Aunt Ezekiel na Shamsa Ford ambao wamekuwa wakimuunga
mkono mgombea urasi wa UKAWA kupitia tiketi ya CHADEMA, Mh Edward Lowassa siku ya jana kwenye Mkutano wa Edward Lowassa na wanawake wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Millenium Tower, mbali na kuelezea kumuunga mkono mgombea huyo mastaa kumzawadia keki ya ‘Birthday’ ya kutimiza 62 ya kuzaliwa ya mgombea huyo.
Akiongea kwenye mkutano huo wolper alitangaza kuanzia jana atakuwa akiitwa Jackline Lowassa na kusisistiza kuwa Lowassa ndiyo Rais wake.
Hakika cha ndimu kimeanza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni