Mlinda
mlango wa Arsenal Petr Cech aliokoa mara mbili mipira ya hatari
iliyokuwa ikielekea langoni mwake na kuisaidia timu yake kupata alama
moja katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool.
Katika mchezo huo mikwaju miwili ya Philippe Coutinho ililenga mwamba huku kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey akikataliwa goli alilofunga kipindi cha kwanza kutokana na kuwa katika mstari wa kuotea.
Cech aliokoa kwa mara nyingine mkwaju wa karibu wa Christian Benteke na kuucheza tena kwa umahiri mpira uliopigwa na Coutinho uliokuwa unaelekea kwenye nyavu.
Juhudi za Alexis Sanchez ziliishia kulenga mwamba kabla ya mlinda mlango wa Liverpool Simon Mignolet kuokoa mkwaju wa Olivier Giroud.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni