Watu wengi siku hizi na haswa vijana huwa wakishahitimu chuoni wanatafuta ajira kwa kipindi kirefu na hatimaye wanakata tamaa.
Wengi hao huamua kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa nia ya kujikimu kimaisha.
Wengi huibukia kuwa wajasiria mali shupavu kutokana na talanta yao.
Aidha wengine uvumbuzi wao huwapatia kipato hata zaidi ya mshahara ambao wangepata laiti wangeajiriwa.
Hata hivyo idadi ya wajasiria mali ambao hushindwa kuendeleza biashara zao baada ya miaka mwili ni kubwa mno.
Je wewe unaweza kuwa mjasiria mali mtajika?
Kupata jibu la swali hilo, tafadhali jibu maswali haya ambayo yatakusaidia kutathmini uwezo wako wa kuwa mjasiria mali shupavu
Tahadhari:
Chemsha bongo hii hailengi kukubashiria iwapo utafaulu au la katika ulimwengu wa biashara.
Imeundwa kutokana na nadharia wala haifai kutumika badala ushauri wa kiufundi.
Je maswali yalikusudia nini ?
Swala zima la ujasiria mali limekuwepo kwa muda mrefu lakini ni hivi majuzi tu ndio utafiti wa kina kuihusu umeanza kufanywa kwa nia ya kutambua mbinu vigezo na tathmini ya ubora wa mjasiria mali na somo lenyewe.
Chemsha bongo hili lilitokana na utafiti wetu wa sera nadharia zilizochapishwa kuhusiana na ujasiria mali kwa ushirikiano na mhadhiri wa chuo kikuu cha Cardiff Metropolitan, profesa Brian Morgan.
Nia yetu ilikuwa kutathmini ushawishi wa mjasiria mali binafsi kisaikolojia ushindani wake na ari ya kutaka kujiendeleza na kujisimamia.
Imeandikwa na Gerry Fletcher, Robert McKenzie, Ransome Mpini, Will Smale, Nzar Tofiq na John Walton.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni