Mlinda mlango wa Manchester United David De Gea ameuambia uongozi wa klabu yake kuwa ''hakutaka kucheza'' kabla ya
kuachwa nje kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya.
Meneja Louis van Gaal hatamtumia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye miaka 24 mpaka dirisha la usajili kufungwa huku kukiwa na uvumi wa kujiunga na Real Madrid. Mchezaji huyo bora wa Man U wa misimu miwili alimwambia kocha wa makipa Frans Hoek kuwa hakuwa tayari kwa asilimia 100.
Mchezaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Romero alianza katika mchezo huo walioshinda dhidi ya Tottenham. De Gea kwa mara nyingine ameachwa nje kwenye kikosi kitakachovaana na Aston Villa ijumaa hii.''Sifanyi maamuzi yote peke yangu,'' alisema Van Gaal.''Nina waalimu wawili wasaidizi pamoja na kocha wa makipa Frans Hoek. ''Fans alikua na mazungumzo na De Gea na amekubaliana na kila kitu kuhusu maamuzi yetu''
Van Gaal amesema kuwa yeye pamoja na benchi zima la ufundi walimtanzama De Gea kwenye mazoezi na kugundua kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid ''siyo yule wa siku zote'
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni