Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro ametimiza umri wa miaka 89 kwa kuandika barua ya
wazi kwa taifa lake.
Barua hiyo ilichapishwa katika gazeti la serikali la Granma ambapo hajazungumzia lolote kuhusu ufunguzi wa ubalozi mpya wa Marekani jijini Havana utakavyofanya kazi na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Badala yake ameituhumu Marekani kwa kuisababishia hasara ya mamilioni ya dola baada ya miaka mingi ya vikwazo vya biashara baina ya nchi hizo mbili.
lakini amezungumzia maridhiano ya kihistoria kati ya nchi yake na Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni