ROSE Donatus Anjelus Ndauka ‘mtata’ amesema kama mwanamke
aliyekamilika na mwenye kuhitaji heshima katika jamii, yupo tayari
kuolewa na kuishi kama mama na mwanaume yeyote.
Akichonga na Amani, Rose alisema japo mume bora anatoka kwa Mungu na
kwamba anangojea aliye chaguo lake, lakini amechoshwa na hali ya kuishi
bila ndoa.
“Mimi kama mwanamke ninayetoka kwenye familia yenye maadili, inafika
wakati natamani kuishi katika ndoa, natamani kuwa na familia yangu na
mume wangu na kwa sasa akitokea yeyote, nikajihakikisha kuwa anavyo
vigezo ninavyovihitaji, hakika niko tayari kuanzisha naye safari ya
maisha,” alisema Rose.
Awali Rose alikuwa na uhusiano na msanii wa Bongo Fleva, Malick
Bandawe ‘King Chiwaman’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja na mwishoni mwa
mwaka jana waliachana.
27 Agosti 2015
Rose Ndauka: Nipo Tayari Kuolewa na Yeyote!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni