Shinikizo la kutaka Pasta mmoja maarufu nchini Kenya akamatwe limeanza kushika kasi baada ya uchunguzi wa mwanzo kuonesha kuwa alikuwa akiendesha gari aina la
Range Rover lililohusika katika ajali ya barabarani na kusababisha kifo cha mama mmoja Mercy Njeri majuma mawili yaliopita.
Kampeini hiyo imeshika kasi kwenye mitandao ya kijamii chini ya kibwagizo#arrestpastornganga na #PastorOfImpunity baada ya tuhuma kuibuka kuwa mtu aliyefikishwa mahakamani kwa shtaka la kusababisha mauaji hakuwa dereva wa gari hilo wakati wa ajali.
Aidha uchunguzi umebaini kuwa maafisa wa polisi wa barabarani katika eneo kulikotokea ajali hiyo walighushi ripoti iliyoandikishwa baada ya ajali na hata kukificha kitabu maalum inayotumika kusajili visa vyote vya trafiki maarufu kama ''OB''.
Sasa jopo maalum la wachunguzi waliotumwa katika kituo hicho cha polisi cha Tigoni wamepigwa na butwaa kupata kitabu kipya cha OB.
''Tumeshangaa sana kuwa kuna kitabu cha ''OB'' ambacho kilifunguliwa tarehe 15 mwezi julai lakini hakina matukio yeyote hadi tarehe 19 ajali hiyo ilipotokea''
Haiwezekani kuwa hivyo ,bila shaka hii ni njama ya kuficha ukweli''
Alisema afisa mmoja anayefuatilia tukio hilo kwa karibu ambaye hakutaka jina lake lichapishwe.
Pasta James Ngan'ga wa kanisa la Neno Evangelism, kulingana na ushahidi wa wale waliofika katika eneo la tukio punde baada ya ajali hiyo ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo la Range Rover akielekea Nairobi kutoka Naivasha.
''Hili gari la lekundu ndilo lilikuwa likijaribu kupita gari lingine la range rover kana kwamba walikuwa wakishindana ndipo akashindwa kurejea upande wake wa kushoto na akamgonga mwenzake ana kwa ana'' alisema mzee mmoja.
''Lakini kwa sababu gari lake halikuwa limeumia sana tulienda kuwaokoa mtu na mkewe ambao gari lao ndogo Nissan March, lilikuwa limeumia sana damu ilikuwa ikitiririka''aliongezea.
Hata hivyo, kitabu cha kunakili matukio ya polisi 'OB' ilikuwa tupu.
Ushahidi huo ulipuuziliwa mbali na badala yake ikadaiwa kuwa hakukuwa na dereva polisi walipofika katika eneo la tukio.
Isitoshe uchunguzi umegundua kuwa mhubiri huyo alikuwa ameandamana na Inspekta wa Polisi wakati wa ajali ambaye sasa imebainika kuwa alikuwa mmoja kati ya walinzi wake ambao sio halali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni