Ni mwanaume kwa kila hali ya siha ila sifa za maumbile yake ni sawa na yale ya mtoto wa miaka 10.
Si jambo la kujivunia kuwa wewe huzeeki ?Hapa duniani watu wengi wanatumia gharama ya juu sana wakijaribu kuzuia wasionekana wamezeeka.
Kama ni wanawake wanajichubua ngozi zao kwa mikorogo, wananunua madawa ambayo yamkini yatawarejeshea mvuto wao !
Kwa kina baba, wananyoa nywele zao zote na ikiwa hakunyoa wanajipaka rangi nyeusi angalau waonekana kuwa bado ni baru baru!
Lakini kwa bwana mmoja mwenye umri wa miaka 26 hali yake ni tofauti sana.
Ana umri wa miaka 26 lakini maumbile yake ni sawa na mvulana mwenye umri wa miaka 10 !
Ni mlevi, ana wachumba wa kike, anavalia nadhifu ila tu sauti yake ni sawa na ile ya mvulana ambaye hajabaleghe.
Kutana na Hyomyung Shin, kutoka Korea Korea Kusini.
Shina anaugua ugonjwa nadra sana unaoitwa, 'Highlander Syndrome'.
Ugonjwa huu unamsababisha, mtu adumae palepale inapompata.
Kwa mfano Shina amesalia kuwa na sura sauti na maumbile ya kijana mwenye umri wa miaka 10.
Anaonekana sawasawa na kijana barubaru.
Anafahamika kama mshiriki wa filamu za miujiza Peter Pan.
Kila mara anaponekana kwenye maonyesho vilabu vya burudani na hata kumbi za disco Shin hulazimika kujihami na kitambulisho chake kinachoonesha kuwa amehitimu umri wa miaka 26.
Shin alizaliwa mwaka wa 1989.
Chumbani kwake kuna picha ya vipusa waliobobea katika Hollywood kama vile Scarlett Johansson, dhihirisho tosha kuwa huenda anandoto ya kukutana na kipusa atakayemuoa siku moja.
Shin aliwahi kushiriki onyesho la televisheni ambalo huwasaidia watu kuimarisha hali yao ya usafi na sura kuambatana na umri wao.
Katika onyesho hilo aliwaomba watayarishaji wamsaidie aonekana kama mtu mwenye umri wake.
Lakini haikufua dafu,,,,,
Hana ndevu na sauti yake ni nyororo utadhania ni mtoto!
Shin,ana kimo cha sentimita 163.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni