15 Agosti 2015

Japan inajutia vita vya pili vya dunia

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso na kujitolea kwa watu wengi wakati wa vita vya pili vya dunia.

Katika hotuba aliyotoa kuadhimisha miaka 70 tangu kushindwa nchi yake katika vita hivyo, Abe ameeleza alichokitaja kuwa kujutia makosa yaliofanywa dhidi ya wanawake ambao walinyimwa heshima zao wakati wa vita.
Amesema Japan inapaswa kuhakikisha kwamba mzozo wa aina hiyo hautokei tena.
Manusura wa vita vikuu vya pili vya dunia mjini Hong Kong wameandamana wakitaka fidia
Bwana Abe ameitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za maadhimishisho ya miaka sabini tangu Japan iliposhindwa vita hivyo
Wakati huo huo kundi la manusura wa vita vikuu vya pili vya dunia mjini Hong Kong wamefanya maandamano nje ya ubalozi mdogo wa Japan kudai fidia kwa kupoteza pesa ambapo wanasema walipata shida kutokana na Japan kuuvamia na kuuteka mji wao .
Hotuba hiyo ilikuwa ya kuadhimisha miaka 70 tangu kushindwa nchi yake katika vita hivyo
Waandamanaji hao wanataka Japan iwabadilishie pesa zao za noti za benki ambazo haitumiki kwa sasa , iwapatie pesa halali .
Wakati wa uvamizi wa Japan wakazi wa Hong kong walilazimishwa kutumia pea zinazofahamika kama YEN za kijeshi mbazo hazikuwa na thamani baada ya vita

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728