Kamati itakayoamua
ikiwa mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, anapaswa kuachiliwa
kutoka gerezani, inatarajiwa kukutana tarehe 18 mwezi ujao.
Waziri wa haku nchini humo, alizuia mwanariadha huyo kuachiliwa siku ya Ijumaa wiki iliyopita kama ilivyokuwa imetarajiwa.
Waziri huyo amesema kuwa uamuzi wa kamati hiyo ya kutoa msamaha wa kumuachilia mwanariadha huyo, baada ya kutumikia kifungo cha miezi kumi ya kifungo chake cha miaka mitano ulitolewa mapema na haina msingi wowote.
Mahakama nchini humo ilimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka wa 2013.
Pistorius alimpigia risasi Steenkamp akiwa bafuni nyumbani kwake mjini Pretoria, baada ya kumshuku kuwa ni mwizi.
Upande wa mashitaka umekataa rufaa ya hukumu hiyo ukisema kuwa Pistorius anapaswa kuhukumiwa kwa mauaji.
Mawakili wa Pistorius wanatarajiwa kuwasilisha nyaraka zao kupinga rufaa hiyo tarehe 17, mwezi ujao, siku moja tu kabla ya kamati hiyo ya kutoa msamaha kukutana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni