Wanasayansi nchini Marekani wamesema kuwa wamefanikiwa kutengeneza chachu yenye vina saba vinavyoweza kupunguza maumivu kwa
kiasi kikubwa.
Chachu hiyo inaweza kubadilisha sukari kuwa hydrocodone dawa inayofanana na morphine ndani ya siku tatu mpaka tano. Kwa sasa inachukua mwaka mzima kuzalisha kundi la dawa za kutuliza maumivu kama hayo kutoka kwenye mmea aina ya popi.
Hata hivyo, watafiti kutoka chuo cha Stanford wamesema kazi zaidi inahitajika kwa sababu utafiti wao umeegemea zaidi kwenye matumizi ya chachu nyingi kutengeneza kidonge kimoja pekee cha kutuliza maumivu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni