RIPOTI ZA MOJA KWA MOJA ZA MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA
18.55pm:Matokeo ya mechi za EPL
Southampton 0 - 3 Everton
Sunderland 1 - 3 Norwich
Swansea 2 - 0 Newcastle
Tottenham 2 - 2 Stoke
Watford 0 - 0 West Brom
West Ham 1 - 2 Leicester
18.51pm:Na Mechi inakamilika ikiwa Tottenham 2 Stoke 2.
18.47pm:Refa anawaita wachezaji waliokuwa wakishikana mashati na anawaonya.
18.45pm:Vijana wa Stoke wazidi kuimarisha mashambulizi yao amini usiamini na mechi inaonekana kuwa ndefu kwa Tottenham.Wachezaji wa timu zote mbili washikana mashati hapa!
18.44pm:Stoke wakosa bao jingine la wazi hapa lo.Tottenham wanakoswa hapa.
18.42pm:Tottenham sasa yajaribu kutafuta bao .Ama kwa kweli mungu si Athumani.Hotspurs walikuwa tayari wanajua wameweka alama tatu kibindoni kabla ya Stoke kusawazisha.
18.41pm:Tottenham 2 Stoke 2
18.40pm:Stoke yasawazisha hapa kupitia Diouf zikiwa zimesalia dakika chache mechi ikamilike.
18.36pm:Stoke wapata bao lao la kwanza hapa dhidi ya Tottenham baada ya mshambuliaji wa Stoke kuangushwa katika lango na hivyobasi refa kutoa mkwaju wa Penalti.
18.20pm:Tottenham wazidi kutamba katika lango la Stoke hapa wakiendelea kufanya mashambulizi.
18.08pm:GOAL - West Ham 1-2 Leicester
Dimitri Payet (55 mins)
Watford 0-0 West Brom
GOAL - Sunderland 0-3 Norwich
Nathan Redmond (56 mins)
18.06pm:Wanafanya mashambulizi hawa wachezaji wa Tottenham katika lango la Stoke. do!.
Sunderland 0-2 Norwich
Tottenham 2-0 Stoke
GOAL - Swansea 2-0 Newcastle-Andre Ayew (52 mins
18.04pm:Kipindi cha pili cha mechi kati ya Tottenham vs Stoke Kinaanza
18.00pm:Matokeo ya ligi ya Ujerumani
Darmstadt 1 : 0 Hannover 96SV
Werder Bremen 0 : 1 Schalke 04FC
Augsburg 0 : 0 Hertha Berlin
Bayer 04 Leverkusen 1 : 1 TSGHoffenheim
FSV Mainz 05 0 : 0 FC Ingolstadt 04
17.55pm: Matokeo baada ya kipindi cha kwanza
Sunderland 0 - 2 Norwich
Swansea 1 - 0 Newcastle
Tottenham 2 - 0 Stoke
Watford 0 - 0 West Brom
West Ham 0 - 2 Leicester
17.47pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Stoke na Tottenham kinakamilika huku Spurs wakiwa wanaongoza kwa bao 2-0
17.46pm:GOAL.Chadli aifungia bao la pili Tottenham baada ya gusa ni guse .
West Ham 0-2 Leicester
17.42pm:Mshambuliaji wa Stoke Diouf akosa bao la wazi hapa baada ya kipa kuokoa lo lo ilikuwa asawazishe lakini bahati haijasimama
17.39pm:Tottenham bado inaendelea kutawala mchezo hapa ingawa Stoke inajaribu kuvamia lango la wapinzani
17.36pm:Mechi inaendelea kati ya Tottenham na Stoke ikiwa bado Tottenham inaogoza kwa bao 1-0.
17.30pm:GOAL - West Ham 0-1 Leicester, shinzi Ozaki aipatia Leicester bao la kwanza dhidi ya West Ham
17.28pm:GOAL - Tottenham 1-0 Stoke.Erick Dier aiweke Tottenham mbele baada ya kona iliopigwa na Mason
GOAL - Sunderland 0-1 Norwich
17.15pm:Swansea inapata bao lake la kwanza kupitia mshambuliaji wake hodari Bafetimbi Gomez.
17.12pm:Watford 0-0 West Brom
Swansea 0-0 Newcastle
Tottenham 0-0 Stoke
Sunderland 0-0 Norwich
17.07pm:Tottenhan inamiliki mchezo hapa.na sasa wanapata mkwaju wa adhabu la la lakini kipa anaokoa kona nyengine.
17.06Pm:Tottenham yafanya shambulizi hapa lakini kipa anautoa na ni kona.
17.04pm:Kiungo wa kati wa Tottenham Dembele aihimili safu ya kati
17.01pm:Tottenhan ambao ndio wenyeji wanaanza mechi kwa kasi huku wakitumai kwamba mshambuliaji wao Harry Kane atafanya mambo katika ngome ya Stoke..
NA MECHI KATI YA TOTTENHAM DHIDI YA STOKE INAANZA
16.45pm:Na Mechi inakamilika huku Everton wakiibuka Kidedea kwa mabao 3-0 dhidi ya Southampton.
16.38pm:Mashabiki wa kilabu ya Southamptom waaanza kutoka uwanjani kabla ya mechi kukamilika
16.37pm:dakika 4 za muda wa majeruhi zaongezwa
16.35pm:dakika ya 90 hapa ikiwa ni dakika za majeruhi.Romelu Lukaku anatoka huku akishangiliwa na mashabikiri wa Everton na badala yake Deulofeu .
16.31pm:Dakika ya 88 Ross Barkley anaipatia Everton bao la tatu hapa na hivyobasi kupiga msumari wa mwisho katika sanduku la Southampton.Barkley alipata pasi murua kutoka kwa Seamus Coleman.
16.29pm:Na mechi ya daraja la kwanza kati ya Burnley dhidi ya Birminghan inakamilika kwa sare ya 2-2
16.25pm:Muda unayoyoma.Wanyama achukua mpira na apiga mkwaju lakini unakosa kulenga goli na unatoka nje
16.24pm:Kipa Tim Howard aokoa hapa hatari kubwa.lo lo karibu Mane afunge hapa
16.23pm:Southampton 0-2 Everton
16.22pm:James McCarthy apewa kadi ya njano kwa kumuangusha Graziano Pelle katikati ya uwanja.
16.18pm:Mshambuliaji wa Southampton Pelle akiwa amekabwa
16.11pm:ligi ya daraja la kwanza
Burnley 2 Birmingham 2
16.08pm:Ligi ya dara la kwanza
Burnley 1 Birmingham 2
16.05pm: Wachezaji wa Everton wamiliki mchezo hapa na wanacheza gusa ni guse kana kwamba tayari wameshinda mechi
16.03pm:Victor Mugubi wanyama ajaribu kumchenga mchezaji wa Everton hapa lakini anakataa kata kata.Kufikia sasa mambo si mazuri kwa Southampton ambayo ilikuwa katika timu zinazoongoza jedwali la Ligi ya Uingereza msimu ulioipita
16.01pm: Oriol Romeu apigwa kadi ya njao hapa baada ya kumchezea visivyo james Macarthy.Kumbuka mchezaji huyu ameingia mda mfupi uliopia baada ya Tadic kutolewa.
15.57pm:Southampton wakosa bao la wazi hapa baada ya Pelle aliyepata pasi safi kupiga mkwaju wa kinyonge uliomlenga kipa Tim Howard.
15.55pm:Kipindi cha pili
Southampton yafanya mabadiliko mawili ili kujaribu kusawazisha.Romelu aingia mahala pa Tadic
15.53:pm-Ligi ya daraja la kwanza Uingereza
Burnley 1-1 Birmingham
15.48pm Tottenham vs Stoke
Je,Harry Kane atavuma dhidi ya Stoke?
Timu ya Stoke itahitaji ushindi wa aina yoyote katika uwanja White Hart lane .Wkiendi ilopita walishindwa 1-0 na Liverpool.
GOAL - Southampton 0-2 Everton
Romelu lukaku ameifungia bao la pili timu ya Everton kunako dakika ya 44 kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza.
3.40pm: Mane
Mshambuliaji wa Southampton Mane afanya mashambulizi katika ngome ya Everton lakini bahati haijasimama.
3:16pm:Burnley 0-1 Birmingham
Mechi ya mapema katika ligi ya daraja la kwanza kati ya Burnley vs Birmingham imetoa bao katika kipindi cha kwanza huku Birminghm ikichukua uongozi kupitia Jon Toral kunako dakika ya 10.
3.08pm:Bao la Everton
Southampton ndio ya kwanza kujeruhiwa katika wikiendi ya pili ya soka ya Uingereza .Baada ya Mane kukosa fursa nzuri ya kuiweka timu yake mbele ,uvamizi uliofanywa na Lukaku na Arouna Kone katika ngome ya Southampton ulimpa fursa Lukaku kucheka na wavu.
2.45pm:-Mechi kati ya Southampton vs Everton
Southampton FC vs Everton FC
Swansea City vs Newcastle United
Watford vs West Bromwich Albion
Tottenham Hotspur vs Stoke City
Sunderland vs Norwich City
West Ham United vs Leicester City
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni