Kundi la wapiganaji wa Boko haram kutoka Nigeria huenda limepunguzwa makali kulingana na rais wa Chad Idriss Deby.
Abubakar Shekau siye kiongozi wake tena baada ya mahala pake kuchukuliwa na Mahamat Daoud ambaye yuko tayari kuanzisha mazungumzo na serikali ya Nigeria, alisema rais Deby.
Katika miezi ya hivi karibuni bwana Shekau hajaonekana katika kanda za video za propaganda zinazotolewa na kundi hilo na hivyobasi kuongeza uvumi kwamba huenda ameuawa.
Mapema mwaka huu vikosi vya Chad vilichukua jukumu kubwa la kuichukua miji na vijiji vilivyotekwa na kundi hilo kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mwaka uliopita ,kiongozi huyo wa Chad alisemekana kutaka kuanzisha mazungumzo na kundi la Boko Haram ambayo hatahivyo hayakufanyika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni