Waandishi wawili wa habari wamepigwa
risasi katika jimbo la Marekani la Virginia wakati wakifanya mahojiano
ya moja kwa moja ya runinga.
Kanda ya video inaonyesha mwandishi wa habari wa kike akimtania mgeni aliyekua akimuhoji kabla ya risasi kufyatuliwa mara nane.
Mwandishi huyo anaonekana akiruka na kamera kuanguka sakafuni huku mwanamume aliyevalia nguo nyeusi na kubeba bunduki akipita karibu.
Kituo kilichoajiri waandishi hao cha WDBJ kinasema mwandishi huyo wa habari Alison Parker na mpiga picha Adam Ward walikufa katika tukio hilo .
Polisi wanasema mshukiwa hajulikani aliko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni