10 Novemba 2014

TAMKO: Ikulu: Tumefedheheshwa Jaji Warioba kushambuliwa

Dar es Salaam. Serikali inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.

Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam Novemba 2, mwaka huu.
“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini wake.
“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”
Kauli hiyo ya Sefue imekuja wakati mdahalo huo uliovunjika baada ya Mzee Warioba kushambuliwa, ukiwa umetangazwa kufanyika upya Jumapili Novemba 16, mwaka huu katika hoteli hiyohiyo.
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole alithibitisha jana kuandaliwa kwa mdahalo huo kuanzia saa 9.00 alasiri siku hiyo.
Tukio la kufanyiwa vurugu Jaji Warioba lililaaniwa na wananchi, wasomi, wanasiasa na wanaharakati mbalimbali wakisema kuwashambulia viongozi na hasa katika mjadala wa Katiba ni kukosa uvumilivu na ni kuashiria machafuko katika siku za usoni.
Balozi Sefue aliongeza: “Najua si jambo zuri, iliwahi kutokea pia kwa Mzee (Ali Hassan) Mwinyi, alipigwa kibao... sasa kingine ni mazingira yanapotokea matukio haya, wakati mwingine ni ngumu.”
Mzee Mwinyi alipigwa kibao Machi 10, 2009 na mmoja wa waumini wa dini ya Kiislamu katika Baraza la Maulidi wakati Rais huyo mstaafu alipokuwa akihutubia.
Kutokana na matukio hayo, Balozi Sefue alisema: “Watanzania tumekuwa na tabia ya kuheshimiana lakini matukio haya yanatokea na kila mmoja hatarajii, kinachotakiwa ni sisi tuwaheshimu wazee wetu hawa.”
Mdahalo wa wiki iliyopita ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, ulivunjika baada ya kutokea vurugu wakati Jaji Warioba alipokuwa akihoji vitendo vya baadhi ya watu kutumia vibaya jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Jaji Warioba alikuwa akihitimisha hotuba yake akichambua hoja zilizomo katika Katiba Inayopendekezwa akilinganisha na zile zilizoachwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiongoza.

Vurugu hizo zilidumu kwa takriban dakika 45 ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli hiyo na msaidizi wake alimtoa ukumbini dakika 30 baada ya sakata hilo kuanza, hali iliyowapa nafasi vijana hao walioonekana kujiandaa kufanya vurugu, kumsogelea Makamu huyo wa kwanza wa rais mstaafu na kumtia msukosuko.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728