Mlipuko wa ugonjwa wa tauni nchini Madagascar umewaua watu 40 na kuwaathiri takriban wengine 80 ,shirika la afya duniani WHO limesema.
WHO limeonya kuhusu hatari za kuenea kwa harahaka ugonjwa huo katika mji mkuu wa Antananarivo.
Hali inaendelea kuwa mbaya kutokana na funza wasiosikia dawa, WHO limeonya.
Binaadamu huambukizwa ugonjwa huo baada ya kuumwa na funza wanaobebwa na panya.
Iwapo ugonjwa huo utajulikana mapema basi huweza kutibiwa kwa haraka.
Lakini asilimia 2 ya visa vya ugonjwa huo nchini Madagascar ni ule hatari unaombukiza mapafu na unaweza kuenezwa kupitia kukohoa.
Kisa cha kwanza cha mlipuko wa ugonjwa huo kilijulikana katika kijiji cha Soamahtamana wilayani Tsiroanomandidy takriban kilomita 200 magharibi mwa Antananarivo mwishoni mwa mwezi Agosti.
Kumekuwa na visa viwili vilivyothibitishwa katika mji mkuu ikiwemo kifo kimoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni