Mtu tajiri barani Afrika kutoka
Nigeria Aliko Dangote amepanda katika watu matajiri katika orodha ya
Forbes ya watu mabilionea ,huku mali yake ikiongezeka na kufikia dola
bilioni 15.4.
Bwana Dangote ameorodheshwa wa 51 duniani ukilinganisha na nafasi ya 67 mwaka 2015 wakati gazeti hilo la Forbes lilipoiweka mali yake kufikia dola bilioni 14.7.
Ni mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement ,ikiwa ndio kampuni kubwa katika uzalishaji wa simiti barani Afrika.
Mtu wa pili kwa utajiri barani Afrika ni raia mwengine wa Nigeria ,Mike Adenua ambaye ana thamani ya dola biloni 10,huku raia wa Afrika Kusini Nicky Oppeheimer akiwa katika nafasi ya tatu na mali yenye thamani ya dola bilioni 6.6.
Gazeti hilo linamuweka Adenua ambaye alitajirika kutokana na mafuta na kampuni za mawasiliano katika nafasi ya 103 katika orodha ya mabilionea duniani huku Openheimer akiwa nafasi ya 103.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni