01 Machi 2016
Nyama ya mbwa yauzwa Ghana
Hilo linafahamika kote duniani iwe ni Afrika, Ulaya ,Marekani na hata kusini mwa Marekani.
Kwa hali halisia kitoweo cha mbwa ni mwiko katika jamii nyingi barani Afrika,,,lakini sio nchini Ghana !
Mwandishi wa BBC wa idhaa ya kiingereza BBC Africa Akwasi Sarpong alipigwa na butwaa alipokuwa katika pita pita zake nchini Ghana alipokutana na wachuuzi wengi tu wakiuza minofu kwa bei nafuu
kandokando mwa barabara za mji wa Kandiga.
Kandiga ni mji mdogo ulioko Kaskazini mwa Ghana.
Kitoweo hicho ambacho ni maarufu Kaskazini mwa Ghana ni kama vile mbuzi wa kuchemshwa ama hata kuku wa kienyeji aliyechemshwa na kuuzwa mitaani na mama ntilie.
Akwasi anasema kuwa kichwa chemsha cha mbwa kinagharimu Cedis 14 sawa na dola tatu na senti 60.($ 3.60)
Mkia wa mbwa unauzwa ghali zaidi cedis 15 ($3.80).
Vipande vingine vidogo vidogo vya nyama ya mbwa aliyechemshwa akawa rojo anauzwa kwa cedi moja.
Amini usiamini!
Walipokuja Wachina barani Afrika wakifuata mali ghafi na kujenga mabarabara na reli kutoka taifa moja hadi lingine ndipo ufahamu kuwa mbwa ni kitoweo murua sana huko kwao ukaanza kujulikana.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni