Kufuatia ongezeko la visa vingi vya
ajali barabarani ,taasisi ya kitaifa ya uchukuzi NIT pamoja na Mamlaka
ya uchukuzi wa ardhini na baharini Sumatra zimezindua mtaala mpya wa
kuwafunza madereva wa pikipiki.
Idadi ya pikipiki nchini Tanzania
imeongezeka kutoka 308,412 mwaka 2010 hadi 1,047,659 kufuatia kuimarika
kwa biashara ya pikipiki.Ukuaji huo hatahivyo umekuwa na athari kubwa za ajali za barabarni huku data iliotolewa na
kamanda wa idara ya trafiki nchini Tanzania Mohammed Mpinga ikionyesha kuwa ajali zinazohusishwa na pikipiki ambazo hutumika kwa uchukuzi hushirikisha asilimia 60 ya jumla ya wagonjwa wanaolazwa katika hospitali kuu ya Muhimbili.
Nchini Tanzania ajali za barabarani ziliwaua takriban watu 3,468 mwaka 2015,ambapo ajali zinazohusisha pikipiki ziko katika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo nchini humo baada ya HIV na Malaria.
Mpinga hatahivyo amesema kuwa pikipiki zitaimarisha viwango vya usalama barabarani kupitia kuvaa kofia za helmet,kutobeba zaidi ya mteja mmoja mbali na kutokunywa pombe wakati mtu anapoendesha.
Vilevile amewaonya wale wanaohusika katika uhalifu akisisitiza usajili wa pikipiki kote nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni