Uchaguzi unafanyika katika nchi tano za Afrika huku Senegal ikiandaa kura ya maoni kupunguza muhula wa rais.
Duru ya pili ya uchaguzi wa urais inafanyika nchini Niger, licha la mgombea upinzani kuwa hospitalini nchini Ufaransa.
Nchini Tanzania katika kisiwa cha Zanzibar, duru ya pili ya uchaguzi wa urais inafanyika baada ya kufutwa kutokana na matatizo yaliyotokea mwezi Oktoba
Uchaguzi pia unafanyika nchini Benin, Cape Verde na Congo Brazzaville.
Rais Muhamadou Issoufou anatarajiwa kushinda muhula wa pili katika kura ya kumpinga waziri mkuu wa zamani na spika wa bunge Hama Amadou.
Wakati wa duru ya kwanza mwezi Februari bwana Issoufou alipata asilimia 48 ya kura huku bwana Amadou akiwa wa pili na asilimia 17.
Usalama ni mkali kisiwani Zanzibar kutokana na kushuhudiwa ghasia wakati wa uchaguzi wa hivi majuzi.
Mwandishi wa BBC kisiwani humo anasema kuwa wapiga kura sio wengi vituoni . Chama cha upinzani cha CUF kimewashauri wafuasi wake kususia uchaguzi huo.
Matokeo ya mwezi Oktoba ya yalikataliwa baada ya mgombea wa CUF Seif Sharif Hamad kujitangaza mshindi kabla ya kutangazwa kwa matokeo rasmi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni