Klabu ya Uturuki Galatasaray
imepigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano yeyote yalioandaliwa na
shirikisho la soka barani ulaya UEFA kwa kipindi cha miaka miwili kwa
kukiuka kanuni za uadilifu wa kifedha
(financial fair play).
Mabingwa hao wa soka ya Uturuki walisajili hasara kubwa iliyolazimu UEFA kuchukua hatua baada ya ufichuzi mwezi Januari.
Galatasaray ilifuzu kwa hatua ya makundi katika kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya msimu uliopita.
Vigogo hao wa soka ya Uturuki wanashikilia nafasi ya 5 hivi sasa katika jedwali la ligi kuu.
Galatasaray, ambayo iliilaza Arsenal kupitia mikwaju ya penalti katika fainali za kuwania kombe la UEFA mwaka wa 2010 wamekuwa wakifuzu kwa mechi za kombe la mabingw barani ulaya katika misimu 4 mfululizo.
Msimu huu wanacheza katika ligi ya daraja la pili yaaani Europa ambapo waliambulia kichapo mikononi mwa Lazio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni