Mamia ya vijana katika jimbo la
Bihar nchini India wamelazimishwa kuvua nguo ili kusalia na suruali zao
za ndani wakati wa mtihani wa kuajiriwa kwa wanajeshi ili kuzuia
kufanyika kwa udanganyifu.
Picha zimeonyesha vijana wanaowania
kuwa wanajeshi wakiwa wamekaa na kukunja miguu katika uwanja mmoja ulopo
mji wa Muzaffar huku wakiwa wamevalia suruali zao za ndani pekee.Jeshi limesema kuwa lilifanya hivyo ili kuhifadhi mda wa kuwachunguza makurutu wengi.
Kurutu mmoja aliliambia gazeti la India Express alihisi kwamba hawakupewa heshima.
Maafisa wanasema kuwa makurutu wapatao 1,159 walishiriki katika mtihani huo wa saa moja wa kujiunga na jeshi la India.
''Wakati tulipoingia katika eneo la Chakkar Maidan,tuliagizwa kuvua nguo zote isipokuwa suruali ya ndani.Hatukuweza kukataa bali kutimiza yaliohitajika licha ya kwamba halikuwa jambo la kawaida''.
Makurutu hao walitawanywa kwa urefu wa futi nane kila upande,Gazeti la India Express lilimnukuu kurutu mmoja akisema.
Gazeti hilo lilimnukuu afisa mmoja wa ngazi za juu katika jeshi akisema kuwa ni makosa kwa utawala kuwafanyia hivyo makurutu hao.
Bihar na maeneo mengine ya India Kaskazini ni maarufu kwa udanganyifu katika mitihani ,mwaka uliopita serikali ya jimbo hilo iliaibishwa baada ya wazazi na marafiki kupigwa picha wakipanda kuta za shule ili kuwapatia majibu ya mitihani wanafunzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni