07 Machi 2016

Kasisi mweusi ajiuzulu Ujerumani


Kasisi mkatoliki mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kati DRC amelazimika kujiuzulu kazi yake nchini Ujerumani baada ya kutishiwa maisha.
Kasisi Olivier Ndjimbi-Tshiende, 66, aliwaambia waumini katika misa ya jumapili katika mji wa Zorneding, iliyoko Munich katika jimbo la Bavaria kuwa amepokea vitisho dhidi ya maisha yake na kuwa hotuba hiyo ndio iliyokuwa yake ya mwisho.
Kasisi huyo ambaye alianza kuhubiri mjini humo mwaka wa 2012.

''Kwa kweli tumepigwa na butwa kufuatia vitisho hivyo dhidi ya maisha ya kasisi Ndjimbi-Tshiende'' taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya kanisa hilo inasema.
Uhasama umeibuka kati ya kasisi Ndjimbi-Tshiende na wanasiasa wa jimbo hilo wanaoshikilia msimamo mkali wa chama cha CSU.
Yamkini kasisi huyo Ndjimbi-Tshiende alitofautiana na kiongozi wa chama hicho cha CSU Sylvia Boher mwezi Oktoba kufuatia matamshi yake.
Boher alikuwa amezungumzia kuhusu uvamizi wa wahamiaji kutoka Eritrea waliokuwa wametoroka kutumikia jeshi la taifa lao.
Baada ya maoni hayo ya kasisi Ndjimbi-Tshiende, mwanasiasa wa chama cha CSU rafiki ya Boher, bwana Johann Haindl, alimtusi kasisi huyo hadharani

Viongozi hao wawili walituhumiwa na umma na wakalazimika kujiuzulu nyadhfa zao chamani.
Chama cha Christian Social Union (CSU) kinamuunga mkono kansela wa Ujerumani Angela Merkel na chama chake cha Christian Democrats (CDU).
Polisi sasa wanaendelea na uchunguzi wa ubaguzi wa rangi na tishio dhidi ya kasisi Ndjimbi-Tshiende.
Ujerumani inakabilia na upinzani mkali dhidi ya hatua ya kansela wa Ujerumani kuwapokea wakimbizi milioni 1.1.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa kasisi huyo ametishiwa maisha mara tano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728