01 Desemba 2014

Siri ya Mizengo Pinda kunusurika yatajwa

Arusha/Zanzibar. Siri ya kunusurika kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow imebainika kuwa wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikubaliana kumwacha kutokana na kubakiza muda mfupi na pia kukwepa kuvunja Baraza la Mawaziri kwa mara ya pili.

Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo walioandaa maazimio manane ya Bunge, Dk Hamis Kigwangalla alisema jana kuwa bila kufikia makubaliano ya kumwacha Pinda, mwafaka usingepatikana baada ya kuwapo makundi mawili yenye kukinzana kuhusu pendekezo la kutaka Pinda awajibike.
“Kama ulivyoona bungeni, wabunge wengi wa CCM, walikuwa wakimtetea Waziri Mkuu, wakitaka asing’oke kutokana na mapendekezo ya PAC, hivyo tukaona ili kufikia maridhiano ni bora kuwaondoa mawaziri na watendaji ambao wameguswa moja kwa moja katika kashfa hii na kumwacha Waziri Mkuu ambaye hakuhusika moja kwa moja,” alisema.
Hata hivyo, alisema kufikia maridhiano hayo, haikuwa kazi rahisi kwani wabunge wa upinzani walitaka mawaziri watimuliwe na Pinda awajibike kwa kuwa ndiye mtendaji Mkuu wa Serikali.
“Kimsingi hakuna sehemu hata moja ambayo Waziri Mkuu ameonekana kuhusika moja kwa moja na sakata hili, ndiyo sababu iliyomfanya abaki salama,” alisema.
Dk Kingwangalla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tamisemi, alisema Bunge lingefanya makosa kama lingeshindwa kuwawajibisha mawaziri hao.
Zanzibar walia na Pinda
Wanasiasa na wanaharakati wa Zanzibar wameelezea kushangazwa na kitendo cha Bunge kumwacha Pinda wakidai kuwa alitakiwa awajibike.
Mwanasiasa mkongwe, Soud Muhanna Nassor (74) alisema kama waziri mkuu Serikali ipo chini yake, alitakiwa kujiuzulu ili kurejesha imani kwa wananchi.
Aliyekuwa mgombea urais wa Muungano kwa tiketi ya TLP 2010, Abdallah Othman Mgaza (70) alisema kimsingi uamuzi uliofanywa na Bunge umezingatia zaidi utashi wa kisiasa badala ya kusimamia kanuni na sheria.
Rashid Salum Adiy (52) alisema licha ya uamuzi uliofanywa na Bunge kutia moyo, Pinda naye alitakiwa ajiuzulu wadhifa wake.
pamoja na mawaziri na watendaji ambao wamehusishwa ili kuendeleza misingi ya uwajibikaji wa pamoja kama alivyowahi kufanya Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728