14 Desemba 2014

Wapinzani walia CCM kuwachezea rafu

Dar es Salaam. Vyama vya CUF na Chadema vimekitupia lawama Chama cha Mapinduzi (CCM) vikidai kimecheza rafu katika mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti viongozi wa vyama hivyo walidai kuwa CCM imekuwa ikicheza mchezo mchafu kwa kuwarubuni na kuwanunua wagombea wake maeneo mbalimbali nchini.
Tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huo mapema mwezi huu, CCM imekuwa ikitupiwa lawama za kuhujumu wapinzani na kwamba inatumia nafasi iliyonayo ya chama tawala kuvikandamiza vyama pinzani.
Hata hivyo, alipotafutwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ili kujibu shutuma hizo zilizotolewa na vyama vya Chadema na CUF alisema: “Siwezi kujibu chochote kwa sababu nyie ninapotoa majibu yangu hamuandiki ipasavyo lakini hao... Mnawaweka kipaumbele. Sasa basi andika walichosema halafu mimi kesho (leo) nitawajibu walichokisema kama kitakuwa na maana.”
Awali, huku akijigamba kuwa na asilimia 85 ya wagombea katika nafasi mbalimbali za uongozi, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu alisema: “Lakini yapo maeneo ambayo dakika za mwisho wagombea wetu ama kwa makusudi ama kwa bahati mbaya wakaingia mitini.”
“Asilimia nyingine zimekuja kupungua kwa hila na njama ambazo zimekuwa zikifanywa na CCM, zikiwamo kununua wagombea wetu, kuwateka, kuwanyanyasa kisaikilojia na maeneo mengine machache ni kutokana na mapingamizi yaliyowekwa ambayo hayakuwa na mantiki,” alieleza Mwalimu.
Kwa upande wake, Kaimu Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mpango na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo alidai kuwa wana uthibisho wa kutosha kwamba CCM kwa kutumia mikono ya Serikali wamejiandaa kuvuruga zoezi la uchaguzi huo ili kupora ushindi, unaoelekea kwenye vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“CCM wameandaa karatasi za kupigia kura zenye alama ya vema kwa mgombea wao ambazo watawapa wananchi waiingie nazo kwenye chumba cha kupiga kura na kuwalipa kati ya Sh5,000 hadi Sh10,000 kwa atakayefanikisha mpango huo,” alisema Mketo huku akiwaonyesha waandishi wa habari mfano wa karatasi hizo na kuongeza:
“Walianza mbinu hizi kwa kuwaengua wagombea wetu ili wa kwao wapite bila kupingwa katika maeneo ambayo Ukawa wana nguvu ila kwa hili la karatasi, tutapambana hadi mwisho.”
Akizungumzia juu ya mwitikio wa kujiandikisha katika zeozi la leo la kupiga kura, Mwalimu alisema kuwa Dar es Salaam imekuwa na mwitikio hafifu kulinganisha na mikoa mingine nchini.
“Mimi nashangaa sana, badala ya watu wa jiji hili kujitokeza kujiandikisha ili waweze kupiga kura na hatimaye wapate viongozi wanaowataka kushughulikia matatizo yao wao wanagoma…Ni asilimia 43 tu ya wakazi wa jiji hili waliojiandikisha kupiga kura leo,” alisema Mwalimu kwa masikitiko.
Alisema watu wengi hawana mwitikio kwa madai kuwa wanashughuli nyingi na wengine wakidai kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unawagusa watu wa vijijini ambako kuna matatizo mengi.
“Watu wanajidanganya. Ukingalia watu haohao ndiyo wanaolalamika tatizo la foleni kila siku na matatizo mengine lukuki, lakini hawataki kujiandikisha ili waweze kupiga kura…Hawafahamu kwamba hao viongozi ndiyo msingi wa suluhu ya matatizo yao,” alibainisha Mwalimu.
Katika hatua nyingine, Mwalimu alisema kwa mara ya kwanza chama hicho kimeweka rekodi ya kuwa na wagombea wengi katika uchaguzi kama wa leo licha ya kukumbana na changamoto lukuki.
“Katika uchaguzi huu Chadema imekuwa na wagombea wengi kote nchini. Tunapozungumza leo (jana), chama chetu kina wagombea zaidi ya asilimia 85, kila kijiji na kitongoji.
Haya ni mafinikio makubwa kwetu. Pia ni majibu kwa wale wanaoeneza propaganda kuwa chama chetu ni cha mjini. Leo nenda kijiji chochote nchini lazima utakuta wagombea wa Chadema…hii ni ishara tosha kwamba tunaenda kupata mafanikio mazuri,”alisema Mwalimu.
Uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa unafanyika huku zaidi ya watu 11,491,661 wakitajwa kujiandikisha kupiga kura leo, tofauti na idadi ya watu 18,587,742 waliotarajiwa kujiandikisha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728