13 Desemba 2014

Zitto apeleka moto wa kufichua ufisadi kwa wawakilishi Z’bar

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amewataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaounda kamati hiyo, kufanya kazi kama ilivyo kamati yake kwa Tanzania Bara.
Zitto aliyasema hayo jana kwenye semina ya wawakilishi hao iliyofanyika jijini hapa ambapo alisema, kamati husimamia matumizi yote ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoidhinishwa na baraza na kutoa taarifa zake kwa Umma.
Alisema hesabu za Serikali huendana na Ripoti ya CAG ambayo ndiyo nyenzo kuu ya Baraza katika kusimamia fedha za umma.
Hata hivyo, Zitto alisema PAC inapoona inafaa, huagiza ukaguzi maalumu kwenye maeneo mahususi na njia hiyo imesaidia kuibuliwa kwa mambo mengi ya ufisadi wa fedha za umma kwa Tanzania Bara.
“Kuna nyakati mkaguzi anakuwa haoni masuala fulani hadi anapoombwa na vyombo vingine na hata wananchi…Ni vyema Kamati ya PAC Zanzibar kutumia pia njia hii ili kuimarisha usimamizi bora wa fedha za umma kwa Zanzibar kama ilivyo sasa katika Jamhuri ya Muungano,” alisema Zitto na kuongeza;
“Ni muhimu kuzingatia kwamba wawakilishi ndiyo chombo cha mwisho katika uamuzi kuhusu masuala ya wananchi wa Zanzibar ikiwamo matumizi ya fedha za umma.”
Ni muhimu kuhakikisha kuwa Wizara ya Fedha ya Zanzibar inajibu hoja za PAC (treasury notes) na hapo ndipo mzunguko wa uwajibikaji unakuwa umekamilika.
Alisema ni wakati wa kufikiria namna ambavyo CAG na PAC wanaweza kutimiza wajibu wao katika kuzuia matumizi yanayoelekea kutokuwa na ufanisi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728