Siku chache baada ya kulaza Manchester United, Stoke City wameandikisha ushindi muhimu Ligi ya Uingereza kwa kucharaza Everton.
28 Desemba 2015
Stoke City, Spurs washinda mechi muhimu
Carrick: Tunacheza kwa ajili ya Van Gaal
Nahodha msaidizi wa Manchester
United, Michael Carrick amelalamika madai kuwa wachezaji wa klabu hiyo
hawachezi vizuri ili kulinda kibarua cha kocha wao.
LVG: Naweza kuondoka mwenyewe Man United
Kocha wa Manchester United Louis van
Gaal amesema kuwa anaweza "kujiuzulu mwenyewe" baada ya Stoke City
kuwapiga magoli 2-0 katika kichapo chao cha nne mfululizo katika
michuano yote.
CCM: Jiwekeni tayari kwa uchaguzi Zanzibar
Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko
hilo limetolewa huku mazungumzo hakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo
kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.Wito wa wafuasi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi ume
Kizingiti mazungumzo ya amani Burundi
Mazungumzo ya kujaribu kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa nchini Burundi yamefanyika nchini Uganda.
Hata hivyo washiriki wamekosa kuelewana kuhusu siku ya kuanza kwa mazungumzo kamili.Wapiganaji waondolewa Syria
Wapiganaji wa makundi ya waasi Syria wameanza kuondolewa kutoka mji wa Zabadani karibu na mpaka wa Syria na Lebanon.
Mbwa aliyeuawa Paris kupewa nishani ya ushujaa
Mbwa wa polisi aliyeuawa wakati wa msako baada ya mashambulio ya Paris atatunukiwa nishani kuu ya ushujaa.
Mlinzi wa Osama bin Laden afariki dunia
Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
20 Desemba 2015
Sanders aomba msamaha kumdukua Hillary Clinton
Image caption
Mgombea anayewania
tikiti ya chama cha Democratic nchini Marekani Bernie Sanders amekiri na
kuomba msamaha kwa aliyekuwa waziri wa mashauri ya kigeni na pia
mgombea mwenza
Bi Hillary Clinton kwa kudukua taarifa za upigaji kura, zilizo tayarishwa na kikosi cha kumfanyia kampeini Bi Clinton.Tishio la 'Bomu' lalazimu ndege ya Ufaransa kutua Kenya
Ndege moja ya
abiria ya Air France Boeing 777 AF463, inayohudumu kati ya Mauritius na
Paris imelazimika kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa
mjini Mombasa - Kenya baada ya kifaa kinachodhaniwa kuwa bomu kupatikana
ndani ya choo cha ndege hiyo.
Gavana aomba msaada wa rais kupitia Facebook
Naibu gavana wa
jimbo la Helmand Kusini mwa Afghanistan amewashangaza wengi kwa
kumuandikia rais wa Afghanistan barua kupitia mtandao wa kijamii wa
Facebook.
Utafiti: Hakuna ugaidi wa kadri au wenye misimamo mikali
Thuluthi moja ya
wapiganaji nchini Syria takriban wapiganaji laki moja wanaiunga mkono
kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State.
Utafiti mpya umebaini kuwa hata kundi la17 Desemba 2015
Vyakula vya kiasili: Matoke
Vyakula vya nyumbani vinapendwa na watu wengi wanaoishi mataifa ya nje na ni moja ya biashara inayoleta faida kwa wanaoifanya.
Wengine wanasema wakila chakula cha nyumbani huwa wanakumbuka mengi na kujiona kama wako walikotoka.
Sikiliza makala hii ya Omar Mutasa kutoka Afrika kusini
16 Desemba 2015
Mshukiwa akamatwa kuhusu mauaji ya Paris
Polisi nchini Ufaransa wamemkamata mwanamume eneo la Paris kwenye uchunguzi wao kuhusu mashambulio ya Novemba 13.
Taarifa kutoka Zanzibar
Taarifa kutoka Zanzibar zinasema boti ya Royal Express iliyokuwa imebeba abiria 367 ikitokea Unguja kuelekea kisiwa cha Pemba imeshika moto ikiwa njiani baada ya injini yake moja kupata
Fabregas: Wachezaji wacheze sawa na mishahara
Kiungo wa kati wa Chelsea amesema wachezaji wa Chelsea wanaolipwa mishahara mikubwa wanafaa kucheza kama wachezaji nyota.
Magufuli amfuta mkuu wa kupambana na rushwa
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Marekani yapandisha riba baada ya miaka 7
Benki Kuu ya Marekani imepandisha kiwango kikuu cha riba kwa alama ya robo ya asilimia.
Ripoti mpya ya UNICEF yashtua
Zaidi ya watoto milioni 16 duniani, wamezaliwa katika mazingira ya kivita katika kipindi cha mwaka mmoja pekee.
Kanisa kuandaa ibada ya Star Wars
Kanisa moja mjini Berlin limetangaza kwamba litaandaa ibada maalum kabla ya Krismasi itakayoongozwa na filamu ya Star Wars.
Yanga yapaa kileleni ligi ya Tanzania
Timu ya soka ya Yanga imerejea tena kileleni mwa ligi ya Tanzania baada kupata ushindi dhidi ya African Sport.
TP Mazembe washindwa tena Japan
Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamecharazwa 2-1 na Club America ya Mexico katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu.
15 Desemba 2015
Utafiti: Uongozi ni ‘hatari kwa maisha
Utafiti uliofanyiwa afya ya viongozi wa mataifa mbalimbali umebaini huwa wanazeeka haraka na kupoteza miaka mitatu katika muda wao wa kuishi kwa sababu ya uongozi.
Shule zote Los Angeles zafungwa ghafla
Shule zote za uma katika jimbo Los Angeles Marekani zimefungwa mara moja kufuatia tishio la usalama.
Mourinho: Naona aibu
Siku moja baada ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho sasa anadai wachezaji wanamsaliti
Leicester waadhibu Chelsea na kurudi kileleni
Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Chelsea wamezidi kutumbukia kwenye matatizo baada ya kupokezwa kichapo cha 2-1 na Leicester City.
Ronaldo, Muller wamo kikosi bora Uefa
Kikosi bora cha wachezaji kumi na moja kilichocheza hatua ya makundi ya michuno ya klabu bingwa ulaya kimetangazwa na Uefa.
Makaburi matatu kuwekwa wi-fi Moscow
Makaburi matatu yanayotembelewa sana na watu jijini Moscow yatawekewa huduma ya mtandao ya wi-fi.
Mahakama yaagiza dawa ya Nurofen isiuzwe
Mahakama moja nchini Australia imepiga marufuku uuzaji wa dawa ya kichwa iitwayo Nurofen.
10 Desemba 2015
Uamsho warejeshwa mahakamani Zanzibar
Mahakama Kuu ya Zanzibar imewaita tena viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ambao wanakabiliwa na kesi ya ugaidi katika mahakama za Tanzania Bara kusikiliza rufaa ya dhamana yao kwa kesi nyengine.
Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu wakiwa kwenye mikutano yao visiwani Zanzibar.
Mwandishi wetu aliye visiwani Zanzibar anasema vikosi vya ulinzi na usalama vimezingira maeneo yote ya Mahakama Kuu ya Vuga na hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani kusikiliza kinachoendelea. Kwa mengi zaidi sikiliza matangazo yetu ya mchana.
Mbwa wa Benjamin Netanyahu huuma wageni
Mbwa ambaye anayefugwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwauma wageni wawili, akiwemo mbunge, katika hafla ya kidini.
Madaktari kupandikiza uume Marekani
Upasuaji umepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kupandikiza uume nchini Marekani, kwa lengo la kuwasaidia mpiganaji wa zamani
Mshindi wa tuzo ya soka ya BBC Afrika kutangazwa
Tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka inayoandaliwa na BBC, itawekwa hadharani hii leo. Mwandishi wa BBC Peter Okwoche ndiye aliyeteuliwa kukabidhi tuzo hiyo na ndiye mwenye bahasha yenye maelezo ya mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu.
Marekani yazidi kuisambaratisha IS
Maofisa wa polisi nchini Marekani wanaoshughulika na mapambano ya kuutokomeza ugaidi, wamesema mkuu wa masuala ya fedha wa kundi la kigaidi la Islamic State ameuawa kutokana na shambulio la anga karibu na mji wa Tal Afar nchini Iraq, katika wiki za hivi karibuni.
Magufuli atangaza baraza la mawaziri
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa sasa lina mawaziri 19, ingawa wizara ni 18. Mawaziri sita kati ya hao ni wanawake.
Mchezaji wa timu ya taifa Honduras auawa kwa risasi
Mchezaji wa timu ya taifa Honduras Arnold Peralta amepigwa risasi akiwa likizoni mji wake wa kuzaliwa wa La Ceiba.
01 Desemba 2015
Xi Jinping ziarani Zimbabwe
Rais wa China Xi Jinping yuko nchini Zimbabwe katika ziara ya siku mbili inayolenga kujenga mahusiano na Zimbabwe.
Waziri wa ulinzi nchini marekani Ash Carter anasema kuwa kikosi maalum cha jeshi la marekani nchini Iraq kitatumwa kuendesha oparesheni kadha dhidi ya Islamic State nchini Syria.
Bwana Carter aliiambia kamati ya bunge la Congress mjini Washington kuwa kikosi hicho kitafanya mashambulazi, kitawakomboa mateka na kuwakamata viongozi wa Islamic State.
Amesema kwa kwa sasa kuna fursa kubwa ya kuwatenganisha wanamgambo wa Islamic State walioko nchini Iraq kutoka wale walio nchini Syria.
Mwezi Oktoba marekani ilitangaza kuwa itatuma hadi wanajeshi 50 maaalum kwenda kaskazini mwa Syria kama washauri kwa vikosi vya waasi wa Kurdi.
Je umetuma picha za utupu kwa simu? Tahadhari
Je umewahi kutuma picha za utupu kwa mpenzi wako ?
Je ulimshawishi akutumie ?
30 wauawa maafisa wa usalama wakipigana Somalia
Shirika la Umoja wa Mataifa linasema watu 40,000 wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya maafisa wa usalama kutoka maeneo mawili.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema watu 30 wameuawa katika makabiliano hayo yanayoendelea katika maeneo ya Galkayo, eneo lililoko katikati ya Somalia na Puntland Kaskazini .
Kumekuwepo mapigano ya muda mrefu ya kiukoo katika maeneo hayo mawili.
Umoja wa mataifa unasema wakimbizi hao wanahitaji vyakula misaada ya matibabu, maji na huduma za usafi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)