Kanisa la Presbyterian nchini
Marekani ambalo lina takriban wanachama millioni 2 ,limebadilisha sheria
yake ya ndoa na kuwajumuisha watu wa jinsia moja.
Kanisa hilo
ambalo linashirikisha idadi kubwa ya wanachama wake duniani lilitoa
tangazo hilo baada ya idadi kubwa ya magavana wa majimbo yake 171
kuidhinisha mabadiliko hayo.Sheria yake mpya sasa itasoma kwamba ndoa ni makubaliano ya kipekee kati ya watu wawili ikilinganishwa na makubaliano kati ya mume na mke.
Mkutano wa makundi katika jimbo la New Jersy ulikuwa wa 86 kuidhinisha sheria hiyo.
Uamuzi huo unatarajiwa kuzua mgawanyiko mkubwa kati ya wanachama wa kanisa hilo ambao wanapinga sheria hiyo.
Mwaka uliopita baraza kuu la kanisa hilo lilitoa idhini kwa wachungaji wake kuwafungisha ndoa wapenzi wa jinsia moja katika majimbo ambayo ndoa hizo zinaruhusiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni