07 Juni 2015

Barcelona waishinda Juventus 3-1

Berlin
Barcelona walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya
fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Berlin
Hatahivyo Alvaro Morata alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya gusa ni guse kati yake na Messy.
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.
Berlin
Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728