11 Juni 2015

Sokwe ni walevi Hodari :Utafiti

Sokwee ni walevi Hodari sana :Utafiti
Sokwe ni binamu wa karibu sana na binadamu.
Sokwe wamekuwa na uwezo mkubwa wa usawa miongoni mwao wnasemekana kufahamu hata njia za
mawasiliano yetu lakini sasa Sokwe ametambulika kubugia mvinyo sawasawa na binadamu.
Watafiti ambao wamekuwa wakiwachunguza sokwe nchini Guinea wamegundua kuwa sokwe wamefanya mazoea ya kukwea minazi na kubugia mvinyo
Utatafiti huo wa miaka 17 umebaini kuwa sokwe hao hutumia matagaa kuchovya ndani ya vibuyu vya mnazi na kisha kunywa.
Kwa wakati mmoja sokwe mmoja alichovya sana buyu la nazi ''hadi akalewa''.
Sokwe wanauwezo wa kuiga asilimia kubwa ya tabia za binadamu
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la ''the Royal Society Open Science'' ulionesha wazi kuwa chokwe wanapenda sana mnazi.
Katika eneo la Bossou nchini Guinea, wenyeji wengi ni wagema wa pombe ya mnazi.
Watafiti hao walipigwa na butwaa sokwe walitumia sponji kutumbukiza ndani ya vibuyu vya mnazi kisha wakanyonya tembo.
Utafiti uligundua kuwa kila sokwe alikuwa akibugia takriban mililita 85 ya pombe hiyo sawa na chupa moja hivi ya mvinyo.
Utatafiti huo wa miaka 17 umebaini kuwa sokwe hao hutumia matagaa kuchovya ndani ya vibuyu vya mnazi na kisha kunywa.
Wengi wao walionesha wazi dalili za kulewa.
Asilimia kubwa ya wale waliobugia pombe hiyo walilewa na kisha kulala.
Dakta Kimberley Hockings kutoka chuo kikuu cha Oxford Brookes na kituo maalum cha utafiti wa wanyama cha Ureno alisema mvinyo huo wa nazi una takriban asilimia 3% ya tembo.
Awali ilidhaniwa kuwa tembo inaweza kuwaua wanyama lakini sasa utafiti huu mpya unaibua maswali mengi tu ambayo bila shaka yanahitaji utafiti zaidi haswa miongoni mwa wanyama wengine, alisema dakta Kimberly.
Kwa hivyo ukipata mnazi wako umepungua kwa kiasi kikubwa usiwe mwepesi kuwalaumu binadamu, labda sokwe wamegundua buyu lako umelificha wapi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728