07 Juni 2015

Nyalandu atangaza kwa mara ya pili kuwania urais


> Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akitangaza nia kwenye Uwanja wa Namfua Mjini Singida. 


Posted  Jumapili,Juni7  2015  saa 9:46 AM
KWA UFUPI
Waziri Nyalandu alitangaza nia hiyo kwenye Uwanja wa Namfua Mjini Singida na mwaka jana alitangazia kwenye mkutano ulifanyika kwenye uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero, Wilaya ya Singida Vijijini.
SHARE THIS STORY
 
 
 
0
Share
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alitangaza kwa nia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao, ikiwa ni mara yake ya pili baada ya kufanya hivyo Desemba 28 mwaka jana.
Waziri Nyalandu alitangaza nia hiyo kwenye Uwanja wa Namfua Mjini Singida na mwaka jana alitangazia kwenye mkutano ulifanyika kwenye uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Ilongero, Wilaya ya Singida Vijijini.
Alichosema jana
Waziri Nyalandu, ambaye aliambatana na mkewe Faraja alieleza mikakati yake kadhaa na kukanusha madai ya baadhi ya wanasiasa kuwa vijana ni mzigo kwa taifa ama bomu linalosubiri kulipuka, badala yake akaeleza kuwa vijana ni fursa muhimu katika maendeleo.
Alisema vijana wakiwezeshwa na kupewa fursa, wataishangaza dunia kwa kuleta maendeleo. Alisema akifanikiwa kuingia Ikulu, atawawezesha vijana na kuwajengea mazingira mazuri ili wajiajiri na waweze kushika usukani wa maendeleo.
Alibainisha kuwa wakati umefika kwa kizazi kimoja kukabidhi uongozi kwa kizazi kingine ambacho ni kipya na kwamba saa ya viongozi wa kizazi kipya imewadia. Aliwaeleza wana Singida kuwa baada ya kuwa Mbunge kwa miaka kumi na tano, ameona sasa ni wakati mwafaka kwake kutaka kuwa kiongozi katika nafasi kubwa zaidi ya Urais.
Vipaumbele vyake
Alieleza kuwa anataka nchi ipige hatua kutoka hapa ilipo kwenda hatua ya mbele zaidi na kwamba taifa litahitaji sera muhimu na makini katika sekta mbalimbali, ikiwamo elimu, afya na nyingine.
Waziri Nyalandu ambaye kabla ya kuanza kuhutubia alipigana mabusu na mkewe kuonesha ishara ya kupendana, alisisitiza kuwa umoja wa kitaifa utalindwa na atapiga vita uonevu, woga, unyanyasaji wa aina zote na dhuluma katika utoaji huduma. Pia alisema atapiga vita ubaguzi na chuki aina zote
Waziri Nyalandu alieleza atatumia nguvu kubwa kuwekeza katika rasilimali watu ambayo alisema ni muhimu kama ilivyo kuongeza nguvu za kuwawezesha watanzania kuwekeza katika jamii.
Nyalandu alimshukuru Rais Kikwete kwa kumuamini na kumpatia fursa ya kumsaidia katika nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii na kueleza kuwa amepata mafanikio makubwa katika nafasi hiyo.
Alisema akiwa msaidizi wa Rais kwenye nafasi hiyo kama Waziri, Utalii ameingiza fedha za kigeni na kukuza uchumi wa nchi huku ukichangia zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa.Alisema watu milioni 2 wananufaika na utalii na kwamba Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika kwa mvuto.
Alisema anaamini nchi bila migogoro ya wakulima na wafugaji inawezekana hivyo ataweka mikakati madhabuti kukomesha mapigano baina ya makundi hayo.
Alieleza kuwa Tanzania kwa mara ya kwanza imefanikiwa katika vita dhidi ya ujangiri na majangiri aliowaelezea kama ni watu wabaya, huku akiweka bayana kwamba mfumo wa hifadhi ya Serengeti kwa Tembo umeongezeka kwa asilimia 98.
Waziri Nyalandu, aliyekuwa akikwepa kutamka neno urais badala yake kutumia neno kuomba Watanzania na wana-CCM wamruhusu aingie malangoni mwao, alitamba kuwa tembo wameongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 katika hifadhi za Tarangire na Manyara, huku idadi ya tembo katika hifadhi ya Selous ikiongezeka kutoka 13,000 hadi 15,000 katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa upande wa hifadhi za Ruaha na Rungwa, alisema bado utaratibu wa kufanyika sensa unaandaliwa idadi yake itajulikana baada ya kukamilika.
Kuchukua fomu leo
Waziri Nyalandu aliyesema kuwa atachukua fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM leo aliwaonya wagombea wenzake kuchunga ndimi zao wanapokwenda kuchukua fomu mjini Dodoma na pia aliwataka kuwa na kauli nzuri na kuwaheshimu wakubwa zao.
Warembo Arusha wahamia Singida
Moja ya vivutio vya tukio la Nyalandu kutangaza nia basi aina ya kosta lililokuwa limebeba wasichana kadhaa kutoka Arusha. Wasichana hao walikuwa wakizunguka mji wa Singida na kusema wamekuja Singida kumsindikiza Waziri Nyalandu.
“Tunapenda Mheshimiwa Nyalandu ndio awe rais baada ya Kikwete ili afanye mambo mazuri zaidi kwa wananchi na Taifa” alisema Roida John.
Kivutio kingine kilikuwa ni helikopta iliyokuwa ikizunguka anga la mji wa Singida, huku mara mbili ikiganda hewani kwa dakika kadhaa na kuwafanya wananchi kushangaa.
Haikujulikana mara moja kama helikopta hiyo ilimbeba Nyalandu lakini ilizunguka uwanja wa Namfua muda mfupi, kabla ya Waziri Nyalandu hajaingia uwanjani majira ya saa 9:57 alasiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728