Nahodha msaidizi wa Manchester
United, Michael Carrick amelalamika madai kuwa wachezaji wa klabu hiyo
hawachezi vizuri ili kulinda kibarua cha kocha wao.
Kocha wa Manchester United Louis van
Gaal amesema kuwa anaweza "kujiuzulu mwenyewe" baada ya Stoke City
kuwapiga magoli 2-0 katika kichapo chao cha nne mfululizo katika
michuano yote.
Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko
hilo limetolewa huku mazungumzo hakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo
kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.
Wito
wa wafuasi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi ume
Image caption
Sanders aomba msamaha kumdukua Hillary Clinton
Mgombea anayewania
tikiti ya chama cha Democratic nchini Marekani Bernie Sanders amekiri na
kuomba msamaha kwa aliyekuwa waziri wa mashauri ya kigeni na pia
mgombea mwenza
Bi Hillary Clinton kwa kudukua taarifa za upigaji kura, zilizo tayarishwa na kikosi cha kumfanyia kampeini Bi Clinton.
Image copyrightAPImage caption
Wataalamu hao wanatoka kikosi cha jeshi la wanamaji wa Kenya na idara ya polisi wa upelelezi.
Ndege moja ya
abiria ya Air France Boeing 777 AF463, inayohudumu kati ya Mauritius na
Paris imelazimika kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa
mjini Mombasa - Kenya baada ya kifaa kinachodhaniwa kuwa bomu kupatikana
ndani ya choo cha ndege hiyo.
Image copyrightEPAImage caption
Afisa huyo Mohammad Jan Rasoulyar alimwandikia rais
Ashraf Ghani kumweleza kuwa wanajeshi 90 wameuawa katika mapigano makali
na wanamgambo wa Taliban
Naibu gavana wa
jimbo la Helmand Kusini mwa Afghanistan amewashangaza wengi kwa
kumuandikia rais wa Afghanistan barua kupitia mtandao wa kijamii wa
Facebook.
Taarifa kutoka Zanzibar zinasema boti ya Royal Express iliyokuwa imebeba abiria 367 ikitokea Unguja kuelekea kisiwa cha Pemba imeshika moto ikiwa njiani baada ya injini yake moja kupata
Image copyrightStatehouse TanzaniaImage captionMagufuli amesema hajaridhishwa na utendakazi wa mkuu huyo
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Image copyrightGettyImage captionTP Mazembe walikuwa wamechapwa 3-0 robofainali
Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamecharazwa 2-1 na Club America ya Mexico katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu.
Image copyrightAFPImage captionShinikizo kutokana na majukumu ya uongozi huenda vinaathiri afya ya viongozi
Utafiti uliofanyiwa afya ya viongozi wa mataifa mbalimbali umebaini huwa wanazeeka haraka na kupoteza miaka mitatu katika muda wao wa kuishi kwa sababu ya uongozi.
Mahakama Kuu ya Zanzibar imewaita tena viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ambao wanakabiliwa na kesi ya ugaidi katika mahakama za Tanzania Bara kusikiliza rufaa ya dhamana yao kwa kesi nyengine.
Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu wakiwa kwenye mikutano yao visiwani Zanzibar.
Mwandishi wetu aliye visiwani Zanzibar anasema vikosi vya ulinzi na usalama vimezingira maeneo yote ya Mahakama Kuu ya Vuga na hakuna aliyeruhusiwa kuingia ndani kusikiliza kinachoendelea. Kwa mengi zaidi sikiliza matangazo yetu ya mchana.
Tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka inayoandaliwa na BBC, itawekwa hadharani hii leo. Mwandishi wa BBC Peter Okwoche ndiye aliyeteuliwa kukabidhi tuzo hiyo na ndiye mwenye bahasha yenye maelezo ya mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu.
Maofisa wa polisi nchini Marekani wanaoshughulika na mapambano ya kuutokomeza ugaidi, wamesema mkuu wa masuala ya fedha wa kundi la kigaidi la Islamic State ameuawa kutokana na shambulio la anga karibu na mji wa Tal Afar nchini Iraq, katika wiki za hivi karibuni.
Image copyrightStatehouse TanzaniaImage captionDkt Magufuli amesema bado anatafuta watu wa kujaza nafasi nne
Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa sasa lina mawaziri 19, ingawa wizara ni 18. Mawaziri sita kati ya hao ni wanawake.
Waziri wa ulinzi nchini marekani Ash Carter anasema kuwa kikosi maalum cha jeshi la marekani nchini Iraq kitatumwa kuendesha oparesheni kadha dhidi ya Islamic State nchini Syria.
Bwana Carter aliiambia kamati ya bunge la Congress mjini Washington kuwa kikosi hicho kitafanya mashambulazi, kitawakomboa mateka na kuwakamata viongozi wa Islamic State.
Shirika la Umoja wa Mataifa linasema watu 40,000 wamekimbia makaazi yao kutokana na mapigano kati ya maafisa wa usalama kutoka maeneo mawili.
Msemaji wa umoja wa mataifa amesema watu 30 wameuawa katika makabiliano hayo yanayoendelea katika maeneo ya Galkayo, eneo lililoko katikati ya Somalia na Puntland Kaskazini .
Kumekuwepo mapigano ya muda mrefu ya kiukoo katika maeneo hayo mawili.
Umoja wa mataifa unasema wakimbizi hao wanahitaji vyakula misaada ya matibabu, maji na huduma za usafi.
Takriban watu 10 wamepigwa risasi na
kuawa baada ya makundi mawili kutofautiana kuhusu jogoo yupi aliyeibuka
mshindi katika vita katika jimbo la Guerrero Mexico.
Kundi la wapiganaji la Islamic State
limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya mashambulio ya mjini Paris Ijumaa
usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Rais Hollande ameelezea
mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa na IS ambao
alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi. Image copyrightPAImage caption
Shambulizi Paris
Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume wanane
waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo katika
sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa.
Papa Francis kurahisisha sheria ya talaka miongoni mwa wakatoliki
Papa Francis
anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki
waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa
katika kanisa hilo .