Balozi Khamis Kagasheki, kazi yake ya kwanza aliifanya kwenye Ofisi ya mwakilishi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kama Katibu.
- Alikuwa ndio amemaliza elimu ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Fordham, kilichopo New York nchini Marekani.
Mapema hapo kesho (29/05/2015), ndiyo tunaanza kurusha rasmi video hizo za mahojiano hapa JamiiForums (Kwa maandishi, audio na Video zitawekwa YOUTUBE Channel) na kwenye WhatsApp kwa watakao taka.
Maswali yaliyoulizwa yalikusanywa na yalipangiliwa katika vipengele husika tokana na maswali ya wadau wa JamiiForums yaliyowasilishwa.
Mkusanyiko wa maswali hayo ulipangwa katika vipengele kumi na sita (16) kila kipengele kikiwa na maswali kadhaa hivyo kufanya kuwe na maswali zaidi ya sabini (70) kwa ujumbla wake. Kwa maana hiyo, hata vipande vya video hizo zimegawanyika katika vipande 70, kila kimoja kikijitosheleza katika sehemu yake.
Kwa wale ambao kuangalia video ni tatizo kwao (vifurushi/kasi ndogo ya mtandao), kutakuwepo na mahojiano hayo katika mfumo wa maandishi pia; hivyo tunawahakikishia kwa kila mmoja atakayependa kujua kilichojiri, ataweza kupata kwa namna moja ama nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni