Mmoja wa makamanda wa ngazi za juu katika jeshi la China ametetea hatua ya nchi hiyo za kuokoa ardhi kutoka baharini katika maeneo yanayozozaniwa kusini mwa china.
Kauli hiyo inawadia siku moja baada ya Marekani kutaka China isitishe mara moja miradi hiyo ikidai kuwa inakiuka maadili ya jumuia ya mataifa huru.
Naibu amiri mkuu wa jeshi la wanamaji la China Su Jianguo aliuambia mkutano mkuu nchini Singapore kuwa miradi huo unalengo la kuboresha uwezo wa nchi yake kutekeleza majukumu yake ya kimataifa na kusaidia eneo hilo.
Alisema kuwa kati ya majukumu hayo ni pamoja na jitihada za uokoaji, utunzi wa mazingira na uhuru wa safari za baharini.
China inadai kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya china ni lake.
Nchi nyingi zinashuku kuwa miradi ina lengo la kuiwezesha China kudai kuwa maeneo makubwa kusini mwa bahari ya china.
Siku ya jumamosi, waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aiitaka Uchina isitishe mara moja mradi wa kuokoa ardhi kutoka baharini.
Carter alisema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
Matamshi yake Carter yanafuatia taarifa ya makao makuu ya jeshi la Marekani iliyodai kuwa Uchina imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo.
Bwana Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi.
Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni