Utumizi wa neno ''uhalifu wa chuki'' ili kuelezea mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la watu weusi mjini Carolina Kusini nchini Marekani umezua mjadala kuhusu ni nini haswa kinachosababisha mtu kutekeleza ugaidi.
Watu wengi wameonyesha hasira zao kuhusu vile afisa mkuu wa polisi mjini Charleston alivyoelezea kisa hicho wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Wanasema kuwa ''uhalifu wa kivita'' sio neno zito linalofaa kutumika kuelezea kisa hicho na kudai kwamba iwapo waathiriwa wangekuwa watu weupe na mshukiwa kuwa mwenye asili ya Asia,ama mweusi neno ugaidi lingetumika.
Mshukiwa Dylan Roof ,mwanamume mwenye umri wa miaka 21 ameshtumiwa kwa kuingia ndani ya kanisa saa tatu za usiku siku ya jumatano na kuwapiga risasi waumini waliokuwa katika maombi.
Katika picha ya mtandao wake wa facebook mshukiwa huyo alikuwa amevalia jaketi lililo na picha na bendera ya Rhodesia na Afrika kusini.
Kanisa la Kiafrika la kimethodisti lina historia ndefu kama eneo la vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na ni muhimu katika historia ya Wamarekani weusi.
Mwanaharakati Martin Luther King na Coretta Scott wote walizungumza katika eneo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni