Timu ya Liverpool iliyo katika ligi kuu ya England nchini Uingereza imeanza harakati za kusaka wachezaji watakaoisaidia kufanya vizuri katika ligi kuu hiyo.
Liverpool ambayo msimu uliomalizika ilionekana kuwa moja ya timu ambazo zingeleta ushindani mkubwa katika kuwania nafasi nne za juu katika ligi kuu hiyo ilijikuta ikiangukia nafasi ya sita.Katika kuimarisha kikosi chake msimu ujao, Liverpool wamejipanga kufanya mazungumzo na mchezaji wa Manchester City, James Milner wiki hii wakati wakikaribia kunasa sahihi ya mchezaji huyo kiungo akiwa mchezaji huru.
Klabu hiyo ya Anfield imempa kipaumbele mchezaji huyo wa kimataifa wa England.
Liverpool inajiamini kuwa itafikia makubaliano na Milner mwenye umri wa miaka 29.
Iwapo mkataba huo utakamilika, Milner - ambaye alijiunga na Manchester City akitokea Aston Villa mwaka 2010 - atajiunga na Wekundu hao tarehe Mosi mwezi ujao.
Milner alianza kuichezea timu ya taifa ya England dhidi ya Uholanzi mwezi Agosti 2009 na amebaki mchezaji wa kutegemewa katika kikosi cha Roy Hodgson.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni