Serikali ya China,imepiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya wazi katika mji wa Beijing. Maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya wazi na watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa faini.
Hata hivyo China ina wavuta sigara milioni mia tatu wakati sheria ya kusitisha wavutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa kutekelezeka.Ripoti inasema kuwa watu wengi wanadhani sheria hiyo ya kukataza kabisa uvutaji sigara haitafanya kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni