20 Juni 2015

Rais Obama akerwa na mauaji Marekani

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Barak Obama amesema mauaji ya watu tisa ndani ya Kanisa la Waafrika Wamarekani katika eneo la
Charleston katika jimbo la Carolina Kusini yanaibua maswali kuhusu sehemu mbaya ya historia ya Marekani.
Katika hotuba yake iliyoonyeshwa katika televisheni muda mfupi baada ya polisi kumkamata mtuhumiwa ambaye ni kijana wa kizungu-- Bwana Obama amesema chuki miongoni mwa jamii kwa misingi ya rangi na imani ni kitisho kwa demokrasia ya Marekani na misingi yake.
Amesema mauaji ya watu wengi hayatokei kwa kiasi hiki katika nchi nyingine zilizoendelea, na ametaka kufanyika kwa mabadiliko ya pamoja katika fikra za Wamarekani kuhusu ghasia zinazosababishwa na matumizi ya silaha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728