Serikali ya Ghana imeahirisha jaribio la chanjo ya ebola inayotarajiwa kujaribiwa katika jimbo la Volta kufuatia hofu kutoka kwa wakaazi.
Taifa hilo halijaathiriwa na mlipuko wa ugonjwa huo Magharibi mwa Afrika,lakini limekuwa likiandaa makao makuu ya kukabiliana na hali ya dharura ambayo yanatarajiwa kufungwa mwezi huu.
Ghana ilikubali kuifanyia jaribio chanjo ya Ebola na wagonjwa waliochaguliwa walifaa kupewa simu za rununu na fedha.
Bunge la taifa hilo sasa limemtaka waziri wa afya kuelezea kuhusu hali hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni