Safari ya mwisho ya ndege ya kwanza inayotumia nishati ya miale ya jua kupaa angani, imetatizika kutokana na hali mbaya ya hewa.
Ndege hiyo iliondoka mapema Jumapili asubuhi mashariki mwa Uchina, katika safari ya siku sita kuelekea Hawahi, lakini safari hiyo imesitishwa baada ya hali ya hewa kuwa mbaya ilipokuwa kwenye anga ya bahari ya Pacific.
Wataalamu wa utabiri wa hali ya anga, wamemuomba rubani wa ndege hiyo kusitisha kwa muda safari hiyo ili kuruhusu hali ya hewa kuwa shwari, ndipo aendelee na safari yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni