Mapigano makubwa yameripotiwa kwenye mji kuu wa Somalia Mogadishu baada ya shambulizi la gari la
kujitoa mhanga kutokea karibu na makao makuu ya idara ya ujasusi ya nchi hiyo.
Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab waliingia jengo lililo karibu na makao hayo makuu ya ujasusi, na kukana madai ya al-Shabab kuwa waliingia makao ya ujasusi yenyewe.
Hakuna ripoti zozote zilizotolewa za watu kuuawa au kujeruhiwa
Al-Shabab wameapa kuongeza mashambulzii dhidi ya serikali ya Somalia wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan ambao ulianza siku ya Jumatano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni