Shirika la ujasusi nchini Marekani FBI linasema kuwa linachungzua ujumbe kwenye mtandao ambao
unaonekana kuandikwa na Dylann Roof, mzungu mweye umri wama miaka 21, ambaye anashutumiwa kwa kuwaua kwa kuwapiga risasi waamerika tisa weusi walipokuwa kwenye mafundisho ya biblia kanisani, kwenye mji wa Charlestion katika jimbo la South Carolina.
Mtandao huo unaoitwa the Last Rhodesian una zaidi ya maneno 2000 ya chuki za ubaguzi wa rangi. Mwandishi wake anasema kuwa Charleston ulilengwa kutokana na historia yake ya utumwa na idadi kubwa ya watu weusi.
Awali mamia ya watu katika mji huo waliandamana kupinga ubaguzi wa rangi na pia kuwakumbuka waamerika hao twa asili ya Afrika ambao waliuawa.
Misa itafanyika leo Jumapili wakati kanisa hilo linafunguliwa tena kwa maombi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni