Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa la kihistoria la Kiafrika katika mji wa Charleston ameshtakiwa na mashtaka tisa ya mauaji pamoja na
shtaka moja la kumiliki silaha, polisi wamesema.
Mshukiwa Dylan Roof mwenye umri wa miaka 21,anatarajiwa kufikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani baadaye hii leo kupitia teknolojia ya video.
Polisi wanayachukulia mauaji hayo katika kanisa la Emanuel AME siku ya jumatano usiku katika mji wa kusini mwa Carolina kama uhalifu wa chuki.
Alikamatwa siku iliofuata yapata maili 200 kutoka mji wa Carolina kazkazini kabla ya kusafirishwa na kurudishwa mjini Charleston.
Gavana wa jimbo la Carolina Kusini Nikki Haley amesema kuwa bwana Roof anapaswa kupewa adhabu ya kifo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni