Maafikiano ya amani yametiwa sahihi yakiwa na lengo la kumaliza mzozo wa miaka mingi kati ya serikali na waasi wa Tuareg.
Serikali imekubali kuwapa madaraka zaidi waasi wa Tuareg na pia imeondoa waranti ya kukamatwa kwa viongozi wake.
Ukiunga mkono makubaliano hayo muungano wa Ulaya umezishauri pande zote kutekeleza majukumu yake na kuitaka serikali kuongoza jitihada na mapatano.
Kikosi cha kimataifa bado kinatafuta njia za kuwadhibiti wanamgambo na makundi mengine yenye silaha yanayoendesha shughuli zao kaskazini mwa Mali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni