Takriban watu 15 wamefariki huko Nepal baada ya maporomoko yaliosababishwa na mvua kubwa kuvizika vijiji sita huko kazkakazini mashariki.
Watu wengi wameathiriika na maporomoko hayo, huku idadi kubwa ya watu ikiwa haijulikani ilipo.
Katika jimbo la Taplejung, afisa wa serikali Surendra Bhattarai, amesema kuwa makundi ya maafisa wa utoaji msaada yamefika katika kingo za mito miwili mikubwa ya Mewa na Tamor, ili kuwatafuta watu ambao walisombwa na maji ya mafuriko.
Nepal,ndio mwanzo inajizoazoa kutokana na tetemeko baya la ardhi lililotokea mwezi wa Aprili na Mei, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nane na mia saba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni